Amber Lulu: Sijawaza Kuolewa, Bado Niponipo!

SEXLADY kunako anga la muziki wa Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber lulu’ ambaye pia ni rafiki wa karibu wa msanii mwenzake Gift Stanford “Gigy Money”, amefunguka kuwa hana mpango wowote wa kufunga ndoa kwani bado anakula bata la ujana.

 

Akizungumza na AMANI, Amber lulu amesema ni kweli ndoa ni baraka, na hakuna mwanamke asiyetamani kuolewa, lakini kwa upande wake bado yupoyupo sana.

 

“Nadhani muda bado haujafikia, nisije nikakimbilia kuolewa nikamtesa bwana harusi, pia siwezi kuolewa eti kisa kuwafurahisha watu wa Instagram, kuolewa ni mipango” alisema Amber Lulu.

MREMBO AJITOKEZA KUHAMASISHA WAREMBO KUOLEWA NA WATU WAZIMA WALIOWAZIDI UMRI..

Toa comment