The House of Favourite Newspapers

Amber Rutty, Bwana’ake Wadaiwa Kuugua Hoi Gerezani!

MSANII Nascat Abubakary ‘Amber Rutty’ na ‘bwana’ke’, Said Mtopari wanaosota Gereza la Segerea jijini Dar kwa kukosa dhamana kufuatia kesi inayowakabili ya kupiga na kuzisambaza picha zao za ngono mtandaoni, imedaiwa kuwa wapo hoi kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu, Ijumaa Wikienda limedokezwa.

 

Mmoja wa ndugu wa washitakiwa hao aliyeomba hifadhi ya jina ameeleza kuwa, wawili hao kabla ya kuswekwa gerezani walikuwa wakiumwa ugonjwa huo na kuna kipindi walizidiwa kiasi cha mwanaume kushindwa kutembea.

 

Ndugu huyo alisema baada ya kuzidiwa, waliwachukua na kwenda kuwauguzia nyumbani kwa wazazi wa mwanaume, Rufuji mkoani Pwani mpaka walipopata nafuu ndiyo wakarudi walikopanga Mtoni Kwa Azizi Ally jijini Dar.

Aliendelea kutiririka ndugu huyo kuwa, wapenzi hao wakiwa kwao ndipo likaibuka sakata hilo la kusambaa kwa picha zao za ngono lililowasababisha wafikishwe mahakamani kisha kusota mahabusu.

 

“Wakiwa huko gerezani hivi karibuni tuliwatembelea na kukuta afya zao kiukweli siyo nzuri yaani wamedhoofu sana na inaonekana kama ugonjwa wao umeanza kuwarudia. Hapa tunajaribu kufanya michakato ya kuwawekea dhamana kama tutafanikiwa,” alisema mmoja wa ndugu hao.

Kufuatia sakata hilo, wanahabari wetu walifika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza nchini na kuzungumza na msemaji wa jeshi hilo, Mrakibu Amina Kavirondo na kumuuliza hali ya washitakiwa hao ambapo maongezi yalikuwa kama ifuatavyo;

 

Ijumaa Wikienda: Kamanda tunataka kujua hali za washitakiwa Amber Rutty na bwana’ake walioko Gereza la Segerea ambao inasemakana wana hali mbaya huko gerezani kufuatia ugonjwa wa kifua kikuu.

Msemaji: Ahaa ninyi ni nani aliyewapa hiyo habari?

Ijumaa Wikienda: Kamanda hizi taarifa zimezagaa mitaani kuwa mahabusu hao wana hali mbaya huko gerezani na hata ndugu nao wametuambia hivyo ndiyo maana tunataka uthibitisho kutoka kwako.

 

Msemaji: Hizo habari mimi sijaletewa rasmi, lakini hata hivyo, kimaadili haturuhusiwi kutoa taarifa za ugonjwa wa mfungwa au mahabusu hadharani hayo ni mambo ya siri.

Si unajua nao ni binadamu hivyo wana haki ya kulindiwa siri zao ikiwemo suala la ugonjwa. Hao wanaowapa taarifa ninyi kwa nini wasilete kwetu tuzifanyie kazi badala yake wanawapa ninyi?

STORI: WAANDISHI WETU, DAR

BEKA FLEVA: Nilihaso Sana Kukutana na Mkubwa Fella

Comments are closed.