The House of Favourite Newspapers

AMEVUNJA MOYO WAKO? SIMAMA, JITHAMINI

HABARI yako msomaji wa kona hii! Ni matumaini yangu kwamba uko poa na unaendelea na majukumu yako ya kila siku. Nakuk aribisha tena jamvini ili tuzun gumze na kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano wa kimapenzi, tukiwa tunaelekea ukingoni mwa mwaka 2018.  Leo nimeamua kuja na mada hii baada ya kusikia malalamiko kutoka kwa wasomaji wangu kadhaa ambao wanalia baada ya kuumizwa na wenza wao kiasi cha wengine kufikia hatua ya kujiapiza kwamba hawawezi tena kupenda.

Unapoz ungumzia suala la maumivu ya mapenzi, japokuwa huumiza sana hasa kama ulikuwa na mapenzi ya dhati na mwenza wako na baadaye akaaamua kukugeuka, siyo suala geni hapa duniani. Unapolia leo kwa sababu ya mapenzi, elewa kwamba mamilioni ya watu wanalia kama wewe ingawa tunatofautiana namna ya kukabiliana na maumivu. Lakini cha kujiuliza ni je, mpenzi wako akikuumiza sana, ni sahihi kujiapiza kwamba hutapenda tena?

Ni sahihi kusema kwamba siku hizi hakuna mapenzi ya ukweli kwa sababu tu amekuumiza? Ni sahihi kusema wanaume wote wako hivyohivyo au wanawake wote ndivyo walivyo? Ukweli ni kwamba, unapovunjika moyo haimaanishi kwamba huo ndiyo mwisho wako wa kupenda, simama, jitathmini kisha anza upya. Unapojiapiza kwamba hutapenda tena au hutamwamini mtu tena, ni makosa makubwa kwa sababu kama uliyekuwa naye ameshindwa kuiona thamani ya penzi lako, yupo ambaye atakuthamini na kukuheshimu.

Kuna usemi maarufu kwamba mlango mmoja unapojifunga, mwingine huwa unafunguka muda huohuo, lakini wengi wetu hupoteza muda mrefu kuutazama ule uliojifunga badala ya kuufuata ule uliofunguka. Msemo huo una maana kubwa kwenye mapenzi kwamba kama mwenza wako amekutenda, amekuvunja moyo, amekusononesha na kukufanya ulie, jua kwamba hakuwa riziki

yako. Huwezi kujua Mungu amekuepusha na nini kwa hiyo badala ya kujiapiza na kukufuru, ni bora ukakubaliana na ukweli, japo huwa inauma sana. Ukishaukubali ukweli, unakuwa kwenye nafasi nzuri ya kupona majeraha ndani ya moyo wako na nakuhakikishia, hata kama ulimpenda vipi huyo uliyekuwa naye, kama amefikia hatua ya kukuumiza na kuuvunja moyo wako, hakuwa riziki yako, endelea kumuomba Mungu kwa sababu yupo ambaye ndiye hasa aliyepangwa kuwa wako.

Upo usemi mwingine kwamba watu wengi huwa hawaoni umuhimu wa kitu mpaka wanapokipoteza na wakati huohuo huwezi kujua ulichokuwa unakikosa mpaka pale utakapokipata. Yawezekana ulimpenda sana, lakini huwezi kujua ulikuwa unakosa nini mpaka utakapokutana na yule mwenye mapenzi ya dhati ambaye atakuheshimu na kukutunzia penzi lako.

Kinachowaumiza wengi huwa ni matarajio makubwa wanayokuwa nayo kwa wenzi wao. Unapomuonesha mwenza wako mapenzi ya dhati, haimaanishi kwamba na yeye atakuonesha kama unavyotaka iwe. Unaweza kupenda sana, lakini ukaishia kulipwa mabaya, kitu cha kuzingatia ni kwamba kama umeamua kupenda, penda kwa moyo wako wote na kama unayempenda ni sahihi kwako, utajikuta nafsi yako ikiridhika na utakuwa na furaha. Unapoweka mategemeo makubwa kwamba mwenza wako naye atakupenda katika kiwango sawa na kile

unachompenda, ikitokea ameenda tofauti, maumivu yake huwa makubwa sana. Jambo la msingi ni kutambua kwamba mwisho wa mapenzi siyo mwisho wa maisha yako, bado unayo nafasi nyingine. Kama umeanguka, simama, jitathmini kwa nini ameuvunja moyo wako kisha anza kujipenda na acha muda uongee, hakika utampata mwingine ambaye atakusahaulisha machungu yote uliyopitia. Kwa leo tuishie hapa, nakutakia maandalizi mema ya sikukuu, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri.

Comments are closed.