The House of Favourite Newspapers

AMKATA SHINGO MPENZI KWA MUNDU AKIDAI ANA MICHEPUKO

PRITESH PATEL (30) kutoka Jimbo la Gujarat, India enzi za uhai wake.

PRITESH PATEL  (30) kutoka Jimbo la Gujarat, India, anashikiliwa na polisi kwa kumuua mpenzi wake, Jyoti Surjeet Singh, kwa madai alikuwa na boifrendi mwingine.

Pritesh Patel (kulia) anayedaiwa kumuua Jyoti Sing akiwa chini ya polisi.

Jyoti  kutoka Mumbai, jimbo la Maharashtra, magharibi mwa India, aliyekuwa  mcheza muziki katika mabaa na mwanamitindo, aliuawa na Patel kwa kutenganishwa kichwa na mwili wake kwa mundu.

Mwili wa Jyoti baada ya kukatwa shingo

Mauaji hayo yanasemekana kufanyika kwenye shamba la Patel katika kijiji cha Timba karibu na jiji la Surat magharibi kwa jimbo la Gujarat. Pamoja na kuwa ameoa, Patel alianzisha uhusiano na Jyoti baada ya kutembelea baa alizokuwa akinengua kuburudisha wateja jijini Mumbai.

 

Inasemekana wawili hao walikuwa pamoja jijini Mumbai, Desemba 27 na 28 walikosherehea Mwaka Mpya kabla ya kurejea Timba Januari Mosi.

Siku iliyofuata, Jyoti alikwenda  kwenye shamba la Patel akiwa na dreva wake, Sandeep Singh na mkewe.  Huko ulianza ugomvi kati ya Patel na Jyoti, ambapo Patel alidai Jyoti alikuwa na boifrendi mwingine.  Katika ugomvi huo,  Patel alichukua mundu na kumkata shingo Jyoti na kukimbia.

Mundu inayodaiwa kutumika kumuua Jyoti

Baada ya kukamatwa, Patel alisema alifanya hivyo kwa kuwa alikuwa ametumia fedha nyingi katika uhusiano wake na Jyoti na kwamba uhusiano na mkewe ulikuwa umevurugika kwa ajili ya mpenzi wake huyo.

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA

Wolper Achumbiwa Rasmi, Mwanaume Mwenyewe, Mh!!!!

Comments are closed.