The House of Favourite Newspapers

TANZIA: MAZISHI YA MPIGA PIGA ATHUMANI HAMISI KESHO

Ratiba ya mazishi.

MWILI wa  aliyekuwa mpigapicha wa magazeti ya serikali (TSN), Athumani Hamisi Msengi,  unatarajiwa  kuzikwa  kesho Januari 5 mchana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.  Mipango ya mazishi hayo inafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza-Madukani,  Mtaa wa Weruweru, Nyumba namba  26.

Aliyekuwa mpigapicha wa magazeti ya serikali (TSN), Athumani Hamisi Msengi enzi za uhai wake.

Marehemu amefariki asubuhi  leo katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili alikofikishwa kwa matibabu baada ya  kuzidiwa ghafla usiku akiwa nyumbani kwake.

Kampuni ya Global Group tunatoa pole kwa wote wanaohusika na msiba huu, tukimtakia marehemu mapumziko ya amani milele.

Comments are closed.