The House of Favourite Newspapers

Amuua Mama Mkwe, Amjeruhi Mkewe Kisha Ajiteketeza Ndani ya Nyumba

Joseph Medadi enzi za uhai wake.

MWANAMUME mmoja Joseph Medadi (32) mkazi wa Kitongoji cha Nyakahanga Kata ya Rusumo Wilayani Ngara, Mkoani Kagera amejiua kwa kujichoma moto ndani ya nyumba baada ya kumuua Mama Mkwe wake kwa kumkata mapanga kisha kumjeruhi vibbaya mke wake sehemu mbalimbali za mwili kwa kumchoma na kisu.

Mwilki wa Joseph Medadi ukiwa kwenye jeneza.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kumkia Machi 17, 2018 ambapo Medadi anadaiwa kumuua Mama Mkwe wake, Elizabeth Simoth anaeyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 na kisha kumjeruhi mke wake Elice Joseph anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28 ambaye amelazwa katika Hospitali ya Murugwanza wilayani Ngara.

Hali ilivyokuwa baada ya mopto kuzima.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Rusumo, Dauson Kadende alisema baada ya Medadi kutekeleza tukio hilo ndipo akachukua uamuzi wa kujichoma moto ndani ya nyumba kwa kutumia mafuta ya petroli hadi kufa.

Nyumba ikiteketea.

Kwa upande wake msemaji wa familia hiyo, Ezeckia Simion alisema chanzo cha tukio hilo ni kuwepo kwa mgogoro wa kifamilia baina ya marehemu Joseph na mke wake.

Aidha, Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilayani Ngara, Abeid Maige amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi juu ya tukio hilo bado unaendelea.

Mwili wa marehemu baada ya kutolewa ndani.

 

Mashuhuda wa tukio hilo.

 

NA MPIGA PICHA WETU | NGARA

Comments are closed.