The House of Favourite Newspapers

ANA UJAUZITO MIEZI SITA, KITUMBO HAKIONYESHI!

Reanna kabla hajapata ujauzito.

REANNA STEPHENS (18) wa Carolina, Marekani,  hivi sasa ni mjamzito wa miezi sita lakini ‘ana bahati’ kwani kitumbo chake hakionyeshi kwamba kina kiumbe anayetarajiwa kuzaliwa baada ya miezi mitatu ijayo.

 

Hali hiyo imemfanya mama-mtarajiwa huyo kukejeliwa na watu kwamba mimba hiyo ni feki na kwamba anachodai ni ujauzito ni kutaka kiki tu.

Akiwa na ujauzito wa miezi mitatu.

Hata hivyo, mwanamke huyo amewashushua watu na kuwaambia kwamba aina ya chakula anachotumia na mazoezi ndivyo vimekifAnya kitumbo chake kisijitokeze kama walivyo wanawake wengine ambao hawapitii mambo hayo.

Reanna atajifungua mtoto wa kiume mwezi wa nne.

Reanna anategemea kupata mtoto wa kiume mwezi Aprili mwaka huu.  Ili kuwadhihirishia wabishi, amepiga picha tatu zinazomuonyesha kabla ya kupata ‘kibendi’ hicho, mieizi mitatu baada ya kuKInasa na miezi sita ambayo imetimia majuzi tu.  Picha hizo zinaonyesha badiliko dogo sana kwa macho.

 

Mama kijacho huyo amewaasa wanawake wengine kwamba wakifuata njia anayoipitia, hawatajikuta na vibendi vikubwa kama ilivyozoeleka, bali watavikwepa na pia kuwa na afya njema.

 

“Nimelinganisha  kibendi changu na wengine katika mtandao wa Facebook, nikagundua kuna tofauti kubwa mno.  Matokeo yake watu wanasema ujauzito wangu ni feki.  Wengine wana wasiwasi na afya ya mwanangu, na wengine wakinishauri niende kumwona daktari haraka,” alisema Reanna alipohojiwa karibuni akiwashangaa wasiomwamini.

 

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/AMASHIRIKA

Comments are closed.