The House of Favourite Newspapers

Anakuumiza au unajiumiza mwenyewe?

0

Couple-in-BedNATUMAI u mzima msomaji wangu, kwa wale wagonjwa niwape pole.

Leo nimekuja na mada mpya inayowahusu wale ambao hawajitambui kama wanaumiza ama wanajiumiza wenyewe katika mapenzi.

Wengi wamekuwa wakiumia mioyo yao kutokana na ama kukosa penzi la kweli au kuingia katika penzi la kitapeli wakiamini ni penzi la dhati. Tatizo hili limekuwa likiwasumbua wengi, inawezekana hata wewe unayesoma makala haya, limewahi kukukuta au upo katika tatizo hili hivi sasa.

Tatizo hili husababishwa na kukosa umakini ikiwa ni pamoja na kutofuata taratibu sahihi kabla na baada ya kuanzisha uhusiano wa mapenzi. Hapa sasa ndiyo chanzo cha matatizo. Mpendwa msomaji wangu, unapokuwa na simanzi ni wazi kwamba kila kitu kitakuwa hakiendi sawa, maisha yanabadilika, kila unachokipanga kinavurugika, ufanisi wako kazini unashuka.

Siyo ajabu, bosi wako anafikiria kukufukuza kazi kutokana na kuboronga ofisini. Kimsingi simanzi ni tatizo sugu katika maisha ya kiuhusiano na ni vyema ikiwa umejifunza mapema jinsi ya kuepuka simanzi katika maisha yako ya kimapenzi.

Kuna mambo mengi ambayo wengi huyakwepa ama kwa kuyajua na wakati mwingine bila kujua kuwa wanakosea na mwisho wanajisababishia simanzi ya moyo.

Katika mada hii nitakupa dawa ya kukuondolea simanzi moyoni mwako. Inawezekana umeshakata tamaa, baada ya kuachwa na kila mwanaume unayeanzisha naye uhusiano ukiamini una mikosi, hapo utakuwa unakosea sana, huna balaa wala nuksi ndugu yangu ni kutojipanga na kutokuwa na utayari wa kukutana na matatizo katika uhusiano.

Hata hivyo, kwa kupitia mada hii kwa makini utaingiza kitu kipya ubongoni mwako na kukufanya uwe mpya katika ulimwengu wa mapenzi.

Kuna wengine wamekuwa wakilia kila siku, inawezekana hata wewe unayesoma mada hii hivi sasa upo katika matatizo makubwa ya kimapenzi na huoni kama kuna sababu ya kuendelea kuishi.

Hapo unakosea sana ndugu yangu, maisha bado yanaendelea, unachotakiwa kufanya ni kujiweka tayari kukabiliana na matatizo yajayo, huku ukihakikisha kwamba huruhusu matatizo ya kujitakia katika maisha yako.

Vipo vipengele vingi ambavyo kwa kuvifuatilia kwa makini utaweza kuondoka katika utumwa wa mapenzi unaousumbua moyo wako na kuharibu taratibu za maisha yako.

KABLA HUJAANZISHA UHUSIANO

Kipengele hiki kinawahusu wale ambao bado hawajaingia katika uhusiano. Hutakiwi kuwa chanzo cha matatizo.

Hapa ni muhimu sana kwako wewe ambaye unatarajia kuingia katika uhusiano mpya. Umuhimu wake unatokana na ukweli kwamba, baada ya kugundua vitu vya kuepuka kabla ya kuingia katika uhusiano itakusaidia kufanya maamuzi sahihi na kuingia katika uhusiano mzuri, wenye mwanga mbele yako.

(i) Tafakari

Simanzi huletwa na mateso ambayo mhusika huyapata akiwa katika uhusiano ambao hakuutarajia. Hii inamaanisha kwamba ama mpenzi uliyenaye hakupendi au wewe mwenyewe umegundua kwamba humpendi!

Hisia hizi zinatosha kabisa kukuingiza katika simanzi ya moyo.

Leo naishia hapa, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine kali.

Leave A Reply