The House of Favourite Newspapers

ANGEL INVESTORS LAZINDUA OFISI ZAKE KIJITONYAMA DAR

Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa ofisi za shirika la Angel Investor, jijini Dar es Salaam,  Salum Shamte (wa pili kushoto) kutoka TPSF akiwa maofisa wa shirika hilo.
Picha ya pamoja.
Picha nyingine ya kumbukumbu.
Baadi ya wageni waalikwa wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.
Wanavyuo walioshiriki katika tukio hilo.
Hafla ikiendelea.

 

 

SHIRIKA la Kimataifa la Angel Investors  (Wawekezaji Malaika) lenye makao makuu  Instanbul, Uturuki,  limefungua ofisi ya Mkuruenzi Mkazi wake nchini kwa lengo la kuwafikia walengwa.

 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkuruenzi Mkazi wa  shirika hilo nchini, Sabetha Mwambenja,  amesema ofisi zake zitakuwa katika  jengo la Millenium Towers, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na Benki ya Covenant.

Akifafanua zaidi ameeleza kuwa Angel Investors imechaguliwa na World Business Angels Investment Forum (WBAF) inayoshirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na Global Partnersip for Final Inclusion (GPFI) ambayo ni idara mojawapo katika kundi la nchi zilizoendelea kiviwanda duniani maarufu kama G 20.

 

Aidha ameeleza kuwa  shirika hiloi linajikita kupeleka huduma za kifedha kwa vijana wasomi, wabunifu, wavumbuzi, wanaoanza biasara na kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kupiga hatua na kuwa wafanyabiasara wakubwa.

 

Ameeleza kuwa WBAF inafanya kazi zake katika nchi zaidi ya 66 duniani, na wajibu wake hapa nchini itakuwa ni kutoa mtaji kuwalea wahusika ambao wanalengwa mpaka kufikia hatua ya kusimama wenyewe, kuwaunganisa na masoko ya huduma na bidhaa walizobuni ama kuvumbua na kuwapa taarifa zinazohusu bidhaa zao kidunia.

 

“Tayari tumeshafanya mazungumzo na sekta ya umma na binafsi vikiwemo vyuo vya elimu ya juu na ufundi kama vile  Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM),  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARco) na vyuo vingine,” amesema Sabetha Mwambenja.

 

Comments are closed.