The House of Favourite Newspapers

CCM YAWASAMEHE ILIYOWATIMUA, YUMO MADABIDA

Wanachama hao waliosamehewa wakiwa wamesimama mbele ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu Mwenyekiti wake, Philip Mangula na Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally na mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) wakati wa Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa leo Desemba 18, 2018 Jijini Dar es Salaam.

 

Kwa kauli moja Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea maombi na kukubali kusamehewa adhabu ya kufukuzwa uanachama kutoka kwa waliokuwa wana CCM wanne ambao walitenda makosa hayo wakiwa Wenyeviti wa CCM ngazi ya Mikoa na Wilaya.

Waliosamehewa na kurejeshewa uanachama ni;

1. Ndg. Ramadhani Rashid Madabida (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam).

2. Ndg. Erasto Izengo Kwirasa (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga).

3. Ndg. Christopher Mwita Sanya (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara).

4. Ndg. Salum Kondo Madenge (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni).

Wanachama hao waliosamehewa wakimshukuru Mwenyekiti wa CCM Dkt. Magufuli, Makamu Mwenyekiti, Philip Mangula na Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) wakati wa Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa leo tarehe Desemba 18, 2018 Jijini Dar es Salaam

 

 

 

Comments are closed.