The House of Favourite Newspapers

Asasi Za Kiraia Zapendekeza Marejesho Sera Ardhi

Beata Fabian Kaimu Mkurugenzi, Haki Ardhi akizungumzia sababu za marejeo ya Sera ya Taifa ya Ardhi ambapo alisema moja ya misukumo ya kubadiri ni pamoja na migogoro ya ardhi iliyopo ni pamoja na wakulima na wafugaji na kusisitiza asasi za kiraia kuendelea kutoa elimu juu ya Matumizi Bora ya Ardhi.

Mratibu wa Mradi wa Ardhi Yetu kutoka CARE International Tanzania, Mary Ndaro akitoa utanguliziwa tamko la Asasi mbalimbali za Kiraia zilizopo Nchini Tanzania juu ya maoni na mapendekezo yanayohusu marejeo ya sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995.

Meneja wa Programu ya ufugaji asili Tanzania kutoka Jumuiko la Maliasili Tanzania akisoma tamko la asasi za kiraia juu ya Marejeo ya Sera ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995.

Naomi Shadrack kutoka Shirika la Kimataifa la OXFAM Tanzania akielezea juu ya namna ardhi inavyoweza kusaidia kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Baadhi ya waandishi wa Habari na wadau mbalimbali wakiwa katika tamko hilo.

Mratibu wa Mradi wa Ardhi Yetu kutoka CARE International Tanzania Mary Ndaro(wa pili kutoka kulia) akijibu swali juu ya jinsi wanawake wanavyoweza kupata Mkopo kwa kutumia ardhi walizonazo.

(PICHA: BONIPHACE NGUMIJE/GPL)

Comments are closed.