The House of Favourite Newspapers

Asha Baraka atoa neno zito mazishi ya mama Banza

0

asha baraka Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka.

GLADNESS MALLYA, AMANI

DAR ES SALAAM: Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka amenena mazito kwenye msiba wa mama wa aliyekuwa mwanamuziki maarufu wa Dansi, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’, Khadija Masanja kwamba watakaa na familia na kupanga jinsi ya kumsaidia mtoto wa Banza, Haji ambaye bibi yake huyo ndiye aliyekuwa tegemeo lake baada ya baba yake kufariki dunia.

majenezaMajeneza yenye miili ya marehemu.

Akizungumza na mwanahabari wetu juzi jijini Dar, Asha alisema kutokana na familia ya Banza kukumbwa na pigo zito la mama yao na mjukuu wake kufariki siku moja ikiwa ni miezi michache tu tangu mwanamuziki huyo naye afariki dunia, atazungumza na familia ili aweze kutengeneza CD ya nyimbo zote za Banza ili iuzwe iweze kumsaidia mwanaye huyo.

banza-mamaMama wa aliyekuwa mwanamuziki maarufu wa Dansi, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’, Marehemu Khadija Masanja (enzi za uhai wake).

“Sisi huwa hatuuzi hatimiliki, tutakachofanya ni kuzikusanya zote na kuziweka kwenye CD na kuuza ili fedha zitakazopatikana ziweze kumsaidia mwanaye kwani bibi yake ndiye aliyekuwa kama mzazi wake kwa mahitaji yote,” alisema Asha.

waombolezajiWaombolezaji wakiwa msibani hapo.

Hata hivyo, Asha alisema endapo wazo hilo litashindikana, watapitisha mchango maalum kwa wadau wa muziki wa dansi ili waweze kupata fedha za kumsaidia mtoto huyo ambaye kwa sasa yupo kidato cha nne ili aweze kusoma kozi yoyote baada ya kuhitimu.

msibaAsha Baraka (katikati).

Dua ya mazishi ya mama Banza na mjukuu wake, Sozi ilifanyika juzi nyumbani kwao Sinza-Lion jijini Dar ambapo simanzi nzito ilitawala kutokana na misiba miwili kwa siku moja na miili yao kuzikwa katika makaburi ya Sinza na kuhudhuriwa na wanamuziki kibao wa bendi za muziki wa Dansi.

chokiAlly Choki (kushoto).

Sozi alikuwa anasumbuliwa na kifua ambapo Jumatatu iliyopita alizidiwa na akiwa anapelekwa Hospitali ya Palestina, alifariki dunia, wakaurudisha mwili nyumbani kwa ajili ya mipango ya mazishi na saa chache baada ya mama Banza kupewa taarifa za msiba, naye alifariki ghafla.

Leave A Reply