The House of Favourite Newspapers

Askari wahitimu mafunzo ya awali Polisi wahaswa kwenda kutoa huduma bora kwa wananchi

0

Waziri wa Mambo yandani ya nchi Mhandisi hamadi Masauni amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameviwezesha vyombo vya ulinzi katika kuongeza idadi ya askari ambao wanakwenda kuimarisha ulinzi na usalama wa Tanzania.

Hayo ameyasema Machi 25,2024 Moshi katika shule ya Polisi Tanzania na Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi wakati akifunga mafunzo ya awali ya askari Polisi katika kambi ya kilele Pori Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro.

Mhandishi masauni amewataka askari kwenda kutoa huduma bora kwa wananchi huku akiwataka kuwa mfano kwa askari watakao wakuta katika Mikoa na vituo vya kazi watapopangiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi wanakokwenda.

Kwa upande wa Kamishna wa Polisi Fedha na Logistiki CP Liberatus Sabas ambaye amemwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini amewataka askari hao wapya kutambua kuwa askari ni kioo cha Jamii ambapo amewataka kwenda kutatua changamoto za wananchi wanaolitegemea Jeshi hilo.

Kamishna wa Polisi Operesheni mafunzo wa Jeshi la Polisi CP Awadhi Juma Haji amebainisha kuwa mafunzo ya kijeshi yanahitaji uvumilivu na nidhamu kubwa ili uweze kufaulu mafunzo hayo ambapo amesema wataendelea kuwafundisha askari hao wakiwa kazini ili kuwajengea uwezo wa kiutendaji.

Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Ramadhan Mungi amesema askari hao wamefundishwa mambo mengi ambayo yamewajenga kitaluma na kijeshi huku akibainisha kuwa wapo wanafunzi ambao wamefukuzwa mafunzo kwa kutokizi viwango vya Jeshi hilo ambao Jumla yao ni 193.

Leave A Reply