The House of Favourite Newspapers
gunners X

Askofu Gwajima, Slaa Waitwa Mbele ya Kamati

0

Spika Job Ndugai ameamuru wabunge wawili, Josephat Gwajima na Jerry Silaa kufika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya bunge.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa cha Bunge, Gwajima anatakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Agosti 23, 2021 saa saba kamili mchana huku Silaa akitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Agosti 24, 2021 saa saba kamili mchana.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa endapo yeyote kati yao atashindwa kufika mbele yakamati hizo kwa muda uliopangwa, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria ya kinga, haki na madaraka ya bunge.

 

Leave A Reply