The House of Favourite Newspapers

ASKOFU KAKOBE AJISALIMISHA UHAMIAJI SAKATA LA URAIA WAKE – VIDEO

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zakary Kakobe akizungumza na waandishi wa habari.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zakary Kakobe amefika katika Ofisi za Uhamiaji zilizopo makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar  kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni mashaka juu ya uraia wake kufuatia barua aliyoandikiwa na mamlaka hiyo Aprili 5, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka katika ofisi hizo, Kakobe amesema kuwa lengo kuu lilikuwa juu ya uraia wake ambapo amewaeleza kuwa yeye ni raia wa Tanzania na mzaliwa wa kijiji cha Kibilizi wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.

 

 

Kakobe amesema ameulizwa pia juu ya cheti cha kuzaliwa na akawambia enzi za kuzaliwa kwake mwaka 1955 vyeti hivyo vilikuwa havitolewi kwani harakati za kuanza kutolewa vyeti vya kuzaliwa zilianza mwaka 1981 hivyo akasema kama watahitaji zaidi chimbuko la  ukoo wake wafike kijiji cha Kanyonza kilichopo Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.

 

Kwa upande wake Naibu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam,  Chrispin Ngonyani,akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya kile walichomuitia Askofu Kakobe, amesema hawezi kueleza kile walichomhoji kwani bado wapo katika hatua za awali za uchunguzi.

Naibu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam,  Chrispin Ngonyani,  akizungumzia tukio hilo.

 

Akizungumza wakati wa mahubiri yake jana, askofu huyo alisema hatikiswi na upepo unaotikisa nyasi huku akiwaasa waumini wake wasimame imara kila wanapokumbana na changamoto na kuongeza kuwa hana hofu kwani wokovu wake siyo wa dhahabu bandia.

LIVE: ASKOFU KAKOBE ATINGA UHAMIAJI KUHOJIWA URAIA WAKE -VIDEO

NA DENIS MTIMA | GPL

Comments are closed.