The House of Favourite Newspapers

Askofu Nkwande: Bungeni Sio Pa Kuzunguzia Utoaji Mimba, Uzazi wa Mpango

0

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Renatus Nkwande amesema bungeni ni mahali patakatifu na si pa kwenda kufanya mzaha na kuzungumza kuhusu uzazi wa mpango, utoaji mimba au mapenzi ya jinsia moja.

 

 

Ameeleza hayo leo Ijumaa Machi 26, 2021 katika ibada ya mazishi ya Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania Hayati John Magufuli inayofanyika katika uwnaja wa Magufuli wilayani Chato Mkoa wa Geita.

 

 

“Bungeni ni mahali patakatifu si mahali pa kwenda kufanya mizaha unakwenda kuanza kuzungumza kuhusu mambo ya uzazi wa mpango, utoaji mimba au mapenzi ya jinsia moja.”

 

 

“Hao wenzetu ambao walitumia hizo njia za uzazi wa mpango wameathirika vizazi kwa vizazi leo hii wanatafuta watoto hawapati licha ya kuambiwa ukizaa mmoja utamtunza ukiongeza wa pili tutamtunza bado mambo yamekuwa magumu,” amesema Askofu Nkwande.

 

Leave A Reply