visa

Aslay, Kopa kukinukisha Pasaka hii Dar Live

KAMA bado ulikuwa ukijiuliza sikukuu hii ya Pasaka uende kiwanja gani basi jibu simpo sana! Mkali wa Ngoma ya Nibebe, Aslay anatarajiwa kushuka Pasaka hii (Aprili 21, mwaka huu) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar akisindikizwa na Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa.

 

Akizungumza na Over Ze Weekend, Mratibu na Meneja wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa, mbali na Khadija Kopa wakali wengine watakaomsindikiza Aslay ni Eazy Man, Young Tusso, Berry Black, Bwax, Osama na Podo.

“Tutakuwa na listi ndefu na hii ni kufanya kila mmoja anaburudika na shoo ya kishindo ndani ya Dar Live. Wengi tunajua kuwa tangu Aslay aachane na Yamoto Band hakuwahi kufanya shoo yoyote pande za Temeke na Mbagala kwa hiyo hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya muziki wa Bongo Fleva.

 

“Niwaombe tu mashabiki kujitokeza kwa wingi katika siku hii ambayo ni ya kihistoria kwani Aslay atapiga nyimbo zake zote kali live kwa kutumia vyombo,” alisema KP Mjomba.
Toa comment