The House of Favourite Newspapers

ATAKAYEMSEMA WOLPER ATAFURAHIA SHOO

Jacqueline Wolper

MKALI wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa siku akimkamata mtu ambaye wanafahamiana vizuri akiwa anamsema kwenye Mtandao wa Instagram atafurahia shoo kwa atakachomfanya.  

Wolper aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, kama mtu mnajuana na ukaona amekosea ni vyema ukamfuata mwenyewe na kumwambia kuliko kuandika unavyotaka Instagram kwani huo ni unafiki.

“Siamini kabisa mtu mwenye mapenzi ya dhati na wewe anaweza kukuandikia ujumbe kwenye Instagram. Mimi huo ninauita unafiki na siku nikimkamata mtu wa aina hiyo atanijua,” alisema Wolper ambaye hakufurahishwa na ujumbe alioandikiwa Wema Sepetu kwenye Instagram na mwigizaji mwenzake, Esha Buhet.

Masaa 3 Lema Kuhojiwa POLISI Kuhusu MO Atoka na Kutema cheche

Comments are closed.