The House of Favourite Newspapers

Aubamayeng Ajiunga Rasmi Barcelona

0

MSHAMBULIAJI nyota wa kiimataifa raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubamayeng hatimaye ameagana na Klabu ya Ligi Kuu Uingereza Arsenal na kujiunga na miamba wa Uhispania, Barcelona.

 

Karibia uhamisho wa fowadi huyo mwenye umri wa miaka 32, kujiunga na mabingwa Catalan ugonge mwamba lakini katika dakika za lala salama makubaliano yalifikiwa na kisha sogora huyo wa zamani wa Dortmund alitia saini mkataba mpya.

 

Kulingana na SkySports, Aubamayeng amejiunga na Catalans kwenye ofa ya bure akiwa amesalia na miezi 18 pekee katika mkataba wake na Arsenal.

Aubamayeng alianza kuvurugana na klabu hiyo Disemba 2021, na kushuhudiwa akivuliwa unahodha. Hatua hiyo ilimchochea kuvimba kichwa na kukataa kuchezea klabu hiyo ya London na kumfanya kuondoka katoka uhamisho wa bwerere.

 

Shangwe nchini Uhispania Awali, iliripotiwa kuwa Pierre-Emerick Aubameyang ametua nchini Uhispania na kuelekea katika Uwanja wa Camp Nou kukamilisha uhamisho wake Barcelona.

 

Hata hivyo, suala tata ambalo lazima lishughulikiwe ni kuhusu nani atalipa mshahara wa Mgabon huyo ikizingatiwa kuwa uhamisho wake ni wa bwerere. Akiwa katika kambi ya Emirates, Aubameyang alichezeshwa michezo 163, kuchangia mabao 113, kufunga magoli 92 na kushinda mataji mawili.

 

Aubameyang ambae hajaichezea Arsenal tangu mwezi Disemba alipoeenguliwa katika kikosi kwa makosa ya utovu wa nidhamu. Barcelona wanatarajia kumtangaza Aubameyang hii leo Asubuhi.

Leave A Reply