AUNT AFUNGUKA KUMSALITI IYOBO

VUNJA ukimya! Baada ya mapichapicha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii yakimuonesha staa mkubwa wa Bongo Movies, Aunt Ezeikiel Grayson akiwa na bwana’ke mpya, mengi yamezungumzwa likiwemo suala la kumsaliti mzazi mwenzake, Moses Iyobo ‘Moze’. 

 

Katika mahojiano maalum (exclusive) na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Aunt au Mama Cookie amefunguka juu ya kumsaliti Iyobo ambaye ni dansa mwenye jina kubwa anayeitumikia Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB).

 

BWANA MPYA

Kwa sasa Aunt anadaiwa kutoka kimapenzi na bwana mpya aitwaye Diallo Alfo, raia wa nchini Ivory Coast au Côte d’Ivoire huko Afrika Magharibi. Wote (Aunt na Diallo), wamezungumza na gazeti hili kwa takriban dakika 30 na kuweka mambo hadharani. Kila mmoja amefungukia uhusiano wake wa kimapenzi na mwenzake baada ya Aunt kuumwaga Iyobo na kuwa gumzo kubwa.

ANAANZA DIALLO

Katika mahojiano hayo, aliyeanza kufunguka ni Diallo ambapo mambo yalikuwa hivi;

MAPENZI YAMEKOLEA

Risasi Mchanganyiko: Umeingia kwenye uhusiano na mwanamke ambaye ni staa mkubwa wa filamu na wewe uko tayari kuwa staa pia?

 

Diallo: Kwanza kabisa mimi sipendi ustaa kabisa, lakini kingine ni kwamba kipindi ninaanza uhusiano na Aunt sikuwa ninajua chochote kuhusu ustaa wake, bali nilijua tu ni mwanamke mzuri na nikamkubali na sasa nimekolea kwenye penzi lake.

Risasi Mchanganyiko: Wakati unaanza uhusiano na Aunt ulijua kuwa tayari ana mtu alikuwa anaishi naye?

ANAJUA MAMBO MAWILI

Diallo: Juu ya Aunt ninajua mambo makuu mawili. Najua aliwahi kuolewa (na Sunday Demonte) na alikuwa na mwanaume ambaye amezaa naye mtoto mmoja na walikuwa wanaishi pamoja.

Risasi Mchanganyiko: Sasa huoni kama umeingilia penzi lao?

Diallo: Hapana kwa sababu wameshamalizana. Kikubwa ninajua ni baba mtoto wake.

 

WAKIKUTANA WATAZIPIGA?

Risasi Mchanganyiko: Je, ukikutana uso kwa uso na Moze itakuwaje?

Diallo: Sitasema kitu kwa sababu hanilipi kodi, hanipi hela ya kula ila tu kama atanigusa na mimi nitamgusa.

ANAMCHEZEA AUNT?

Risasi Mchanganyiko: Una mpango wa kumuoa Aunt au ni uhusiano ya muda mfupi au unamchezea tu?

Diallo: Siwezi kusema kuhusu kumuoa Aunt sasa hivi ni mapema mno, lakini pia kwa nchini kwetu ni lazima mwanamke akubalike kwa wazazi, wamjue vizuri kabisa.

 

AUNT WA NNE?

Risasi Mchanganyiko: Mbona kuna tetesi kuwa umeshaoa huko nchini kwenu?

Diallo: Wanaosema hivyo hao ni watu wa mitandaoni ila hakuna shida, maana mimi ni Muislam ndiyo maana ninasema hakuna shida atakuwa ni wa nne.

AUNT NAYE

Baada ya kuzungumza na mwanaume huyo mpya wa Aunt, Risasi Mchanganyiko lilimgeukia Aunt na kufanya naye mahojiano juu ya sakata hilo. Katika mahojiano hayo, Aunt alifunguka kama ifuatavyo;

Risasi Mchanganyiko: Ni kitu gani kilichokufanya ukamwagana au kumsaliti Moze na sasa tayari una mwanaume mwingine?

Aunt: Siwezi kuzungumza kuhusu hilo, lakini kuna wakati huwa vitu vinaisha na unaangalia maisha mapya ndivyo ilivyotokea kwenye maisha yangu.

 

COOKIE VIPI?

Risasi Mchanganyiko: Kwa hiyo huyu ndiye mpenzi mpya sasa? Vipi kuhusu mtoto wako na Moze (Cookie)?

Aunt: NdiYo kama unavyoona (Aunt akijibebisha kwa Diallo). Kuhusu mtoto, Moze ataendelea kuwa baba mtoto wangu na nitamheshimu kwa hilo kwa sababu hatujaachana kwa ugomvi.

Risasi Mchanganyiko: Baadhi ya watu wanasema kama ni mapema mno kumwanika mwanaume wako mpya kwenye mitandao ya kijamii, je, unaonaje?

Aunt: Inawezekana wengine wakaona ni mapema, lakini kwangu najua siyo mapema.

 

ALIKUTANA WAPI NA DIALLO?

Risasi Mchanganyiko: Ulikutana wapi na Diallo?

Aunt: Siwezi kuzungumza hilo na ningependa niishie hapo.

STORI: IMELDA MTEMA, RISASI MCHANGANYIKO


Loading...

Toa comment