The House of Favourite Newspapers

Aunt Amuachia Mungu!

HAKUNA kitu kibaya kwenye maisha kama kupokonywa tonge mdomoni, wakati mwingine unaamua kufanya kama alivyofanya staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel kwa kumuachia Mungu mtihani uliomkuta wa kufungiwa pub (baa) yake ya The Luxe iliyokuwa Mikocheni A jijini Dar.

 

Kumekuwa na sababu nyingi za kufungiwa kwa baa ya Aunt, lakini kubwa zaidi ni kufungulia muziki mkubwa na kusumbua majirani wakati wa usiku huku ikielezwa kuwa, nyumba aliyoikarabati na kufungua baa hiyo miezi miwili iliyopita, ina kesi mahakamani.

 

Aunt ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, kuna wakati unafika anashindwa kuongea chochote kuhusiana na mtihani huo mkubwa alioupata kwani alitumia gharama kubwa kukarabati nyumba hiyo, kulipa kodi na kuweka mtaji wake mkubwa kiasi cha kufilisika baada ya kufungiwa biashara yake hiyo.

 

Aunt amesema kuwa, jambo hilo ameamua kumkabidhi Mungu ili amsaidie na kumtia nguvu kwani kwa nguvu zake mwenyewe hawezi kuhimili uzito wake.

“Hivi ulishamuona mtu amefika sehemu kwenye maisha yake akashindwa kufanya lolote?

 

“Hiyo ndiyo hali niliyonayo kwa sababu hata kuinua mdomo niseme chochote naona ni ngumu sana. Mimi sasa hivi nimeamua kumuachia Mungu kila kitu kuhusiana na pub yangu, yeye ndiye atakuwa mtetezi wangu na atasimama badala yangu,” alisema Aunt kwa uchungu.

 STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Comments are closed.