The House of Favourite Newspapers

Aunt Kujifungua Akirushwa Laivu

0

UKISTAAJABU ya Musa, utaona ya firauni! Ndivyo unavyoweza kutafsiri maajabu anayotarajia kuyafanya Staa wa filamu Bongo, Aunt Greyson Ezekiel baada ya kuweka wazi kuwa, amenuia kuongozana na mashabiki zake leba, pindi atakapokuwa akijifungua.

 

Akizungumza na Risasi Jumatano, Aunt alisema mwaka huu lazima aongozane na mashabiki wake wote wanaomfuatilia kwenye mitandao ya kijamii, runinga na njia nyingine.Alisema ujauzito wake wa kipindi hiki, amependelea ‘kushare’ na mashabiki zake, yote aliyoyapitia.

 

“Nimewaonyesha watu kuwa, sio kila ujauzito ni wa kuhuzunika nataka wanawake wote wafurahie wanapokuwa katika hali hii.

 

“Kipindi hiki wataona ‘live’ kuanzia naingia leba mpaka najifungua, na wataona siku hiyohiyo nitabahatika kupata mtoto gani,” alisema.

 

Alisema kupitia app ya Swahiliflix, mashabiki hao watajionea kila kitu, na wanachopaswa ni kuwa na bando la kutosha la intaneti, kwa sababu kitakachofanyika siku hiyo, kitakuwa na historia ya kipekee kwenye maisha yake.

 

“Siku hiyo mpaka baba wa mtoto wangu ataonekana live, hakuna kitu ambacho kitafichika kwenye ujauzito huu, na ndiyo maana mpaka sasa naliachia tumbo langu wazi.

 

“Mimba ya Cookie naamini hakuna aliyeliona tumbo langu likiwa wazi hata kidogo, lakini kipindi hiki nimelionyesha live, sijalificha na nitaonekana live wakati wa kujifungua,” alisema Aunt ambaye ni Mama wa mtoto mmoja aliyezaa na dansa maarufu wa Diamond, Moses Iyobo kabla ya kutengana.

STORI NA IMELDA MTEMA, RISASI 

Leave A Reply