The House of Favourite Newspapers

Aunty Lulu Achekelea Kuanza Mwaka Vizuri

Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.

MWANADADA asiyeishiwa matukio Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amejikuta akitoa meno yote nje baada ya kuanza mwaka 2018 vizuri kwa kuwa na duka la vitu vya warembo.

 

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Aunty Lulu alisema anamshukuru Mungu kwa kumaliza mwaka 2017 salama japo ulikuwa na changamoto nyingi, lakini 2018 utakuwa wa mafanikio kwani anamiliki duka la nywele na urembo wa wanawake maeneo ya Salasala, Mbezi Beach jijini Dar.

 

“Namshukuru Mungu kwa kila kitu na niwaambie tu watu kwamba usimdharau mtu maana hakuna aijuaye kesho, nimeanza mwaka kwa furaha na shangwe maana kwa sasa ninamiliki duka na mwaka huu naamini utakuwa wa mafanikio sana kwangu,” alisema.

MAGAZETI JAN 3: Hii Ndiyo Sala ya Babu Seya na Magufuli Walipomtembelea Ikulu

Comments are closed.