The House of Favourite Newspapers

AUNTY LULU AMPONGEZA MAKONDA MSAKO WA MASHOGA

Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’

SIKU chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kutangaza oparesheni ya kuwasaka wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja ‘mashoga’, msanii wa filamu, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amempongeza kwa hatua hiyo.

Aunty Lulu aliiambia Za Motomoto News kuwa, amefurahishwa mno na hatua aliyoichukua Makonda kwani naye ni mmoja wa mastaa waliokuwa wakiishi na mashoga, lakini Mungu akamuokoa na kuachana nao hivyo zoezi hilo litasaidia kwani mashoga hao wamesababisha hata wanawake wasiolewe.Image result for MAKONDA

“Ninampongeza sana Makonda maana hawa mashoga ni janga la kitaifa, naomba akishawakamata wakipimwa na kugundulika wanafanya ufuska huo, wakusanywe kwenye uwanja mkubwa wachapwe viboko baada ya hapo ndiyo wapelekwe gerezani kwa sababu wanawake tunakosa kuingia kwenye ndoa kwa sababu yao,” alisema Aunty Lulu.

Hata hivyo, alimuomba Makonda azungumze na Rais John Pombe Magufuli ili msako ufanyike kwa nchi nzima kwani mashoga wengi wamekimbia jijini Dar na kwenda mikoani.

Stori: Gladness Mallya, Dar

Comments are closed.