The House of Favourite Newspapers

CHOKI AANZA MAZOEZI RASMI

Ali Choki

BAADA ya kuugua kwa mwezi mmoja na siku kadhaa, hatimaye mwanamuziki wa Dansi, Ali Choki ameanza mazoezi ya muziki katika bendi anayoifanyia kazi ya Super Kamanyola iliyopo jijini Mwanza.

Akizungumza na Risasi Vibes, Choki alisema alianza mazoezi rasmi wiki iliyopita ikiwa ni baada ya madaktari wake kumweleza kuwa kwa sasa amepona kwa asilimia 80 hivyo anamshukuru Mungu na Watanzania waliokuwa wakimwombea wakati akiwa hoi.

“Tayari nimeshaanza rasmi mazoezi ya muziki ila kupanda jukwaani bado maana ninakula kwanza ugali wa kisukuma na sato nipate nguvu za kutosha na mwisho wa mwezi huu mambo yakiwa mazuri ndiyo nitaanza kupanda stejini kuwaburudisha mashabiki wangu,” alisema Choki

Stori: RISASI VIBES

Comments are closed.