The House of Favourite Newspapers

Aussems Aitoa Mapinduzi Cup Akilini Mwake

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema yupo visiwani hapa kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi, lakini katika kalenda yake, kombe hilo halipo.

Aussems alisema amekuja Zanzibar na kikosi chake kamili, lakini kutokana na ratiba kubana, anaiwaza zaidi michuano ya kimataifa.

Patrick Aussems

Simba ikiwa Zanzibar, leo Ijumaa itacheza mechi ya kwanza ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Chipukizi, huku ikifahamu kuwa, Januari 12, itakuwa na mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika Hatua ya Makundi dhidi ya JS Saoura ya Algeria.

Stori na Kazija Thabit

Comments are closed.