The House of Favourite Newspapers

Aweso Akutana na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Msuya

0

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso akiwa mkoani Kilimanjaro amefika kwenye Makazi ya Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Cleopa Msuya Wilaya ya Mwanga ikiwa ni ratiba ya kuelekea eneo la Mradi wa kimkakati wa Maji wa SAME-MWANGA-KOROGWE ambapo limefanyika tukio la kihistoria la kukwamua shughuli za ujenzi na utekelezaji wa Mradi huo.

 

Waziri Aweso amempa Mzee Msuya taarifa ya hali ya Utekelezaji wa Mradi pamoja na mipango na dhamira iliopo katika kuhakikisha Mradi huo unakamilika.
Aidha imekua fursa kwa Viongozi wa Wizara, Mkoa, Wilaya na Chama kupata nasaha, kupokea ushauri maoni, busara na mawazo kutoka kwa Waziri Mkuu mstaafu na zaidi kupata historia ya ujenzi wa Mradi huo ambayo anaifahamu vema.

 

Katika hatua nyingine Waziri Aweso leo tarehe 13 Machi 2023 ameshuhudia tukio la kuhuisha Mkataba na kukabidhi eneo la site kwa wakandarasi kuiendeleza kazi iliobakia ili kukamilisha mradi wa Same-Mwanga-Korogwe.

 

Leave A Reply