The House of Favourite Newspapers

Aweso Kumwakilisha Rais Samia Kwenye Jukwaa la Maji Duniani Nchini Indonesia

0

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Hamidu Aweso (Mb) leo Aprili 30, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Tri Yogo Jatmiko kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Kongamano la 10 la Jukwaa la Maji Duniani litakalofanyika kuanzia tarehe 19-20 Mei, 2024 nchini Indonesia.

Aidha, Waziri Aweso amefanya mazungumzo hayo na Balozi Tri Yogo Jatmiko Jijini Dodoma na kuiomba Indonesia kushirikiana na nchi yetu katika maeneo ya uwekezaji wa miradi mikubwa ya maji, kuwajengea uwezo wataalamu katika sekta ya maji, teknolojia ya upatikanaji wa mita za maji za malipo kabla (pre-paid meter) na katika eneo la uendelezaji wa Rasilimali za maji.

Kwa upande wake Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mhe. Tri Yogo Jatmiko amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali mwaliko wa kushiriki katika Kongamano hilo la 10 la wadau wa sekta ya maji Duniani ambalo lina fursa nyingi katika uwekezaji kwenye sekta ya maji, utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa vyanzo vya maji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan atawakilishwa na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Hamidu Aweso katika Kongamano hilo la 10 la Jukwaa la Maji Duniani.

Leave A Reply