The House of Favourite Newspapers

AZAM FC WAPOKELEWA KWA MBWEMBWE DAR NA KOMBE LAO (PICHAZ + VIDEO)

Mashabiki na wachezaji wakinyanyua Kombe lao la Mapinduzi.

Baada ya kumaliza kazi kisiwani Unguja, kikosi cha Azam FC kimewasili jijini Dar es Salaam, asubuhi ya leo na kupokelewa na mashabiki wengi wa timu hiyo.

Walivyotua na Kombe.

Azam FC imetwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa mara ya pili mfululizo baada ya ushindi wa penati 4-3 dhidi ya URA ya Uganda kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 usiku wa jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kombe likiwa ndani ya gari la Azam.

Fainali hiyo ilihudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein, ambapo shujaa wa Azam FC alikuwa ni kipa, Mghana Razack Abalora aliyepangua mikwaju miwili ya URA.

Basi la timu ya Azam likiwa na wachezaji wa timu hiyo.

Katika bandari ya Dar, wachezaji, viongozi na benchi la ufundi la Azam FC walionekana kuwa na furaha huku kukiwa na shangwe nyingi kutoka kwa mashabiki ambao baadhi yao walikuwa wamevaa jezi za timu hiyo na kushangilia kwa nguvu.

Comments are closed.