The House of Favourite Newspapers

Azam Marine, Kilimanjaro Fast Ferries Zasitisha Safari za Zanzibar

KAMPUNI ya Azam Marine na Kilimanjaro Fast Ferries, kupitia Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA),  imesitisha safari zake kati ya Dar es Salaam na Zanzibar kuanzisha leo Oktoba 23, 2018, kutokana na hali mbaya ya hewa baharini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mamlaka Ya Udhibiti wa Hali ya Hewa (Zanzibar), safari hizo  zitarejeshwa na mamlaka husika na hali ya baharini itakapotulia.

Kwa wanaotaka maelezo zaidi wawasiliane na kampuni za Azam Marine na Kilimanjaro au wafike katika ofisi zao.

Comments are closed.