The House of Favourite Newspapers

Azam Yaruhusu Sure Boy Kutua Yanga

0

UONGOZI wa Klabu ya Azam umesema uko tayari kumuuza kiungo wao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kwa Yanga au klabu yoyote inayomuhitaji kama wataenda mezani na kuafikiana kuhusu dau la mchezaji huyo.

 

Sure Boy amecheza kwa mafanikio makubwa katika kikosi cha Azam FC kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 sasa huku kukiwa na taarifa ya Yanga kuhitaji huduma yake.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ alisema kuwa wao wako tayari kumuuza mchezaji huyo, hivyo wanamkaribisha yeyote anayemtaka.

“Tunasikia kuwa kuna baadhi ya timu zinamuhitaji mchezaji wetu Salum Aboubakar, ila sisi tunachojua ni kuwa bado mchezaji huyo ana mkataba na Azam lakini hilo haliondoi uwezekano wa kumpata kwa klabu yoyote inayomuhitaji.

 

“Unajua kuna wakati wachezaji wanaweza kuvutiwa na mkakati fulani kutoka klabu nyingine jambo ambalo linakubalika, hivyo kama Yanga watakuja mezani tukazungumza na mchezaji mwenyewe akaridhia basi sisi hatuna kipingamizi tutaruhusu aende,” alisema Zaka Zakazi.

 

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema: “Kwa sasa niwatoe hofu mashabiki na wapenzi wa Yanga kuwa mambo mazuri yanakuja ila waendelee kuwa na subira kila kitu kitakuwa wazi.”

Stori: Joel Thomas, Dar es Salaam

Leave A Reply