The House of Favourite Newspapers

AZMA: NILIKACHA CHUO IFM KWA SABABU YA MUZIKI

0

 ngoma ya Astara Vaste na Garagasha

Kama umeshawahi kusikia au kuiona ngoma ya Astara Vaste na Garagasha, basi jina la Rapa Azma anayewakilisha Jiji la Mbeya, litakuwa siyo geni masikioni mwako, aliwahi kuacha chuo IFM, alipokuwa akisomea masomo ya uhasibu, ili aweze kupata muda wa kufatilia kazi zake za muziki.

Azma ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayoitwa Kidedea, aliyorekodi nchini Kenya, amesema kuwa;

 ngoma ya Astara Vaste na Garagasha
“Baada ya kuona kazi zangu za muziki hazifanyi vizuri, nikaamua kusimamisha masomo yangu kwa muda ili nishughulike na muziki tu, nilivyojiridhisha kwamba sasa muziki wangu ni tishio mjini, nikarudi tena chuo na kuendelea na masomo, ambapo mwaka jana nimefanikiwa kumaliza.

“Kwa kipindi nilichosimama chuo, nilihakikisha nautumia muda wangu vizuri kukuza muziki wangu, nimefanikiwa kuachia ngoma ya Kidedea ambayo nilirekodi nchini Kenya, lakini pia nimefanya kolabo na msanii mkubwa nchini Kenya anaitwa Gilad, ambayo itatoka hivi karibuni. Kwa sasa mashabiki wangu waendelee kuburudika na Kidedea,” amesema Azma.

NA ISRI MOHAMED/GPL

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Sikiliza Hadithi za Mtunzi Eric Shigongo Hapa

Leave A Reply