The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kudaiwa Alishafariki, Anayedai Kuwa Baba Mzazi wa Young Killer Kajitokeza (Video)

INASTAJAABISHA, kusikitisha na kuhudhunisha! Hivi ndivyo unavyoweza kusema kutokana na wazazi wengi hasa upande wa kiume kuwapachika mimba wanawake na kuwatelekeza kisha mwisho wa siku anakuja kudai mtoto baada ya kuona amefanikiwa.

 

Hii imemkuta Rapa maarufu hapa Bongo anayetokea Rocky City, Mwanza, Erick Msodoki ‘Young Killer’ mzee Bujiku ambaye anayedai kuwa ni baba yake mzazi amejitokeza LIVE na kufanya mahojiano maalum na Kipindi cha Global Entertainment.

 

Kwa mujibu wa Baba huyo, ambaye ni mzaliwa na mwenyeji wa mkoani Mwanza ambako ndiko hasa anapotokea Rapa Young Killer, anadai alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mama mzazi wa Rapa huyo, akampachika mimba na kumtelekeza kutokana na kukosa uwezo wa kumlea kwa wakati huo kwa sababu alikuwa bado mikononi mwa wazazi.

 

“Nilikuwa na uhusiano na mama yake Young Killer, nikawa nimempachika ujauzito, aliponieleza nilikataa nikasema siwezi kuwa na mtoto kwa kipindi kile kwani nilikuwa naishi kwa wazazi, nafanya kazi za saluni na yeye alikuwa akifanya kazi kwenye nyumba za watu, (kazi za ndani). Niliaamua kuhamia Dar es Salaam kutafuta maisha.

 

“Nilianza kumuona Young Killer kwenye magazeti baada ya kuanza kazi zake za mziki, kwa kuwa nina mtoto wangu anajulikana sana kwa jina la Msodoki, na yeye Killer anaitwa Modoki, nikaenda kufuatilia hadi Mwanza kwa ndugu na jamaa zangu niliowaacha kule ndipo nikapata ukweli kuwa Young Killer ni mwanangu.

 

“Sikuweza kumtafuta mama yake kwa kuwa sijui huenda alishaolewa na mme mwingine naweza kuleta ugomvi wa familia yao, lakini pia hata Young Killer sijamueleza kwa kuwa sijui kama atanipokea na kuamini kuwa mimi ndiye baba yake mzazi.

 

Young Killer, alishwahi kuhojiwa na kusema tangu azaliwe hajawahi kumuona baba yake na amekuwa akisikia taarifa tofauti tofauti kuhusu baba yake kitu kinachomchanganya na kushindwa kufanya maamuzi ya kumsaka baba yake na kwamba hajui ukweli ni upi, kwa hiyo mpaka sasa mama yake ndiye ana mchango mkubwa wa kumlea bila msaada wa mtu yeyote.

 

Aliongeza kuwa mama yake amekuwa akimpa mahitaji anayoyahitaji kipindi chote cha malezi kitu kilichofanya asiwe na sababu ya kutaka kujua zaidi baba yake yupo wapi.

Fuatilia Mkasa huu wa kusisimua na utoe maoni yako

Comments are closed.