The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kufikia Makubaliano, Graham Potter Akubali Kuinoa Chelsea

0

 

MMILIKI wa Chelsea Todd Boehly alikutana na Potter katikati mwa London Jumatano alasiri kwa kile kilichoelezwa kuwa “mazungumzo chanya” kuhusu meneja huyo wa Brighton kujiunga na klabu yake ya Chelsea huko Stamford Bridge pamoja na mipango ya kuendeleza shughuli nzima ya soka.

Graham Potter

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya Chelsea kumtimua aliyekua kocha wake Thomas Tuchel ambaye hajafanya vizuri katika mechi za hivi karibuni.

 

Majadiliano hayo yaliendelea mapema Alhamisi asubuhi, kwa kuzingatia maelezo ya kisheria ya mkataba wake na wafanyakazi waliopo nyuma Potter.

Graham Potter akaribia kujiunga na Chelsea

Bado hakuna mikataba iliyotiwa saini, hata hivyo pande zote mbili zimefikia makubaliano ya mdomo kuhusu kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 kuchukua mikoba ya Thomas Tuchel ndani ya Stamford Bridge.

 

Imeandikwa:Dunstan Erick kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply