The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kusota Sero kwa Siku Mbili, Babu Tale Aachiwa

MKURUGENZI wa Kampuni ya Tip Top Connection na Meneja wa Diamond Platnumz, Hamis Taletale maarufu Babutale ameachiwa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam tangu jana Alhamisi na sasa yupo uraiani japo haijafahamika iwapo yupo nje kwa dhamana au vinginevyo.

 

Tale alifikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar, juzi Jumatano Mei 23, 2018 kufuatia kesi yake anayodaiwa na Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Tsh. Milioni 250 ambapo kesi hiyo iliahirishwa baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata kutokuwepo mahakamani hapo.

 

Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde, baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

 

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi, katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyewalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.

 

Comments are closed.