The House of Favourite Newspapers

Baada ya Mwaka Mpya, Mbowe na Wenzake Warejea Tena Mahakamani

0
Mahakama kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi No 16, 2021 yenye mashtaka ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe na wenzake watatu inaendelea leo Januari 10 mwaka 2022.
Kesi hiyo inarejea  kutoa fursa kwa Mahakama kupokea ama kutopokea ushahidi wa sare za Jeshi na ramani ya vituo vya mafuta kama ilivyowasilishwa na shahidi wa nane katika kesi hiyo.
Hiyo inatokana na Shahidi wa nane kwenye kesi ya Msingi namba 16 ya Mwaka 2021 Jumanne Malangahe kumaliza kutoa ushahidi wake nakuiomba mahakama ipokee vithibitisho hivyo ambavyo alidai kuvikamata kwa mshitakiwa wa kwanza Halfan Bwire kwenye kesi hiyo viwe sehemu ya ushahidi wake.
Kwa upande wa Utetezi ukiongozwa na wakili Peter Kibatala walipinga Mahakama isipokee sare za Jeshi, ikiwemo ramani ya kulipua vituo vya mafuta ambapo shahidi wa nane alidai kuvikamata kwa mshitakiwa Bwire baada ya kukamatwa eneo la Rau Madukani Mkoani Kilimanjaro.
Mawakili wa utetezi kwa pamoja waliomba Mahakama isipokee vielelezo hivyo kwa madai kwamba shahidi Jumanne Malangahe kwa upande wa jamhuri ameshindwa kuonyesha mlolongo wa ukamataji (Chain of Custody)wa vitu hivyo hadi kufikishwa Mahakamani.
Pia walidai kwamba katika maelezo yake shahidi hakuweza kutoa maelezo ya kutosheleza kuthibitisha iwapo sare hizo ni za Jeshi la  Wananchi wa Tanzania (JWTZ) au la!
Ikumbukwe kuwa hata hivyo Jaji Joachim Tiganga ambaye anasikiliza shauri hilo baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili aliahirisha shauri hilo hadi leo Januari 10 mwaka 2022 kwa maamuzi madogo.
Leave A Reply