The House of Favourite Newspapers

BAADA YA PRINCE DYLAN, MOBETO SASA KUZAA MAPACHA!

0

Ukisikia mfanyabiashara Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ anakosa usingizi, basi ujue ni kwa sababu ya mwanamitindo Hamisa Mobeto, ambaye amechepuka na ‘baby’ wake hadi kunogewa kiasi cha kumzalia mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Prince Dylan, na sasa amesema ana mpango wa kumuongezea watoto wengine mapacha.

Mobeto amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Snapchat kuwa anatarajia kutafuta watoto mapacha tena anapendelea zaidi awe wa kike na wa kiume.

Mashabiki wanadai kwamba hizo ni mbwembwe tu, zile za ‘jishebedue mke mwenziyo akujue’, anafanya hivyo ili amrushe roho Zari.

NA ISRI MOHAMED/GPL

Leave A Reply