The House of Favourite Newspapers

BABA MZAZI AFICHUA MAZITO YA AMBER RUTTY – VIDEO

AR ES SALAAM: Baba mzazi wa mwanamitindo Nascat Abukary ‘Amber Rutty’, Abubakary Abdul Milenga, mkazi wa Bomba Mbili Songea, ameibuka na kueleza mambo mazito yamhusuyo binti yake, Amani limezungumza naye.  

 

Amber Rutty na jamaa yake, Said Mtopari ambao wanatuhumiwa kujirekodi na kusambaza video ya ngono, wapo mahabusu Segerea baada ya kushindwa kulipia bondi ya dhamana ya shilingi milioni 15 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, wiki iliyopita.

 

TUMSIKILIZE BABA SASA

Akizungumza na Amani kwa zaidi ya dakika 45 kwa njia ya simu, baba Amber Rutty, alisema kuwa anaumia sana kwa kile kilichomtokea mwanaye huyo hadi kufikia hatua ya kusambaa kwa picha zake chafu ambazo mpaka sasa hajui ni kitu gani kilimpata mpaka kuamua kufanya hivyo kutokana na jinsi alivyomlea kwenye maadili ya dini.

 

KUMBE ANAONGOZA MSIKITI

Baba huyo alifunguka kuwa, kinachomuumiza zaidi, yeye ni kiongozi wa Misikiti wa Bomba Mbili, na hakuna ambaye hamjui Shekhe Abukary na pia anafundisha madrasa kijijini pale hivyo kusambaa kwa picha hizo kumemuathiri kwa kiasi ambacho anashindwa hata kutembea mitaani.

“Hapa nilipo sipati usingizi hata kidogo na toka picha zianze kusambaa sili chakula vizuri, nagusa kidogo naacha kila nikifikiria hilo tatizo la mtoto wangu na mimi ni kiongozi wa msikiti jamani….,” alizungumza kwa huzuni baba Amber Rutty.

AANIKA HISTORIA YAKE

Baba huyo alizidi kufunguka kuwa mtoto wake huyo alimzaa 1987, akiwa na ndugu watatu waliozaliwa pamoja lakini kwa bahati mbaya zaidi mama yao alifariki 1993 na kuwaacha wakiwa wadogo hivyo alihangaika kuwalea mpaka alipooa mke mwingine ambaye alimsaidia kulea.

“Kiukweli Amber Rutty, mama yao alikufa akiwa mdogo sana nimewalea kwa shida mno lakini baadaye nilipata msaidizi ambapo nilioa mke mwingine ambaye aliwalea kama watoto wake kabisa wa kuwazaa,” alisema baba huyo.

 

AZIDI KUFUNGUKA

Baba huyo alizidi kufunguka kuwa, Amber Rutty alipofikisha umri wa miaka saba, alimuanzisha Shule ya Msingi Bomba Mbili na alikuwa mtoto mwenye maadili mazuri ya Kiislamu na huku akiwa haachi kichwa chake wazi mpaka alipomaliza darasa la saba ambapo alifaulu vizuri.

Alisema licha ya kufaulu, alishindwa kuendelea na masomo kwa sababu shule aliyokuwa amechaguliwa ilikuwa mbali sana hivyo walimkataa. “Mtoto wangu ilikuwa huwezi kukiona kichwa chake, alikuwa ni mtoto mwenye akili nyingi sana shuleni mpaka akafaulu lakini alishindwa kuendelea kwa sababu ya umbali wa shule,” alisema baba huyo.

 

KUMBE ALIOLEWA

Baba huyo alieleza kuwa, binti yake huyo alipendana na kijana anayeitwa Ally Rajabu, ambaye alifunga naye ndoa mwaka 2009, nyumbani kwake na wakaishi kijijini hapo kidogo kisha wakahamia na mume wake jijini Dar na kubahatika kupata watoto wawili wa kike na wa kiume lakini mwaka 2015 alisikia wameachana.

 

ALIJARIBU KUWASULUHISHA

Baba wa msanii huyo alizidi kueleza kuwa, alipokea taarifa za mwanaye kuachana na mumewe na kila mtu anakaa kivyake, akajaribu kuwasuluhisha lakini ilishindikana hivyo hakuwa na namna.

“Kila siku swala zangu ilikuwa ni kwa mtoto wangu ili warudiane na mumewe wawalee watoto wao kwani ni wadogo sasa na kila wakati nilikuwa nikipokea mashtaka nawasuluhisha lakini haikuwezekana, wakaachana, mara ndio nikasikia hili tena la picha chafu,” alisema baba huyo.

ATAMANI KUMUONA MWANAYE

Baba huyo aliendelea kufunguka kuwa, anatamani sana kufunga safari hadi Dar, kwa ajili ya kusikiliza kesi ya mtoto wake lakini kutokana na hali duni hawezi kuja na pia ana matatizo ya kifamilia.

“Naumia sana kusikia mwanangu amekosa hata wa kumdhamini lakini mimi mwenyewe ningetamani nije Dar ila uwezo wangu mdogo, namuomba sana mheshimiwa Paul Makonda, awaangalie tena kwa jicho la msamaha watoto hao,” alisema baba huyo.

 

Baada ya gazeti hili kumsikia baba wa Amber Rutty, lilifunga safari mpaka Mbagala Kiburugwa, alipokuwa akiishi Amber Rutty na kuonana na kaka wa bwana wa Amber Rutty, Saidi Mtopea, Hemed Bakary na kusema kuwa yeye hajui la kufanya ili kuwasaidia mdogo wake na mpenzi wake.

“Hapa unaponiona nimechanganyikiwa sijui la kufanya kabisa, familia yetu ni duni mno bondi ya dhamana waliyopewa ni kubwa na kila unayemwambia anaonekana kukwepa suala hilo na pia Amber na mwenzake ni wagonjwa, walikuwa wanatumia dawa kwa muda mrefu ndio wamemaliza hivi karibuni sijui hata huko jela inakuwaje jamani,” alisema kaka huyo huku akitokwa machozi.

MAMA MWENYE NYUMBA ANENA

Mama mwenye nyumba wa Amber Rutty, aliyejulikana kwa jina la mama Zena, alisema kuwa amempangisha Amber Rutty na mpenzi wake lakini hawakuwahi hata siku moja kumvunjia heshima.

Mama huyo alisema kuwa, Amber Rutty ni mtu mstaarabu na anaongea na kila mtu hivyo hata yeye alishangaa kuona zile picha mtandaoni.

 

“Siwezi kusema baya juu ya huyu dada maana kwa kweli ni mstaarabu na anamheshimu kila mtu hapa mtaani, mimi tangu nilivyompangisha hatujawahi kukwazana wala hajawahi kugombana na yeyote ila hapa nikijaribu kuwahusisha watu kuhusiana na kumsaidia naona kila mmoja anachenga na hiyo bondi ya dhamana ni kubwa mno,” alisema mama huyo.

 

MJUMBE NAYE ANENA

Mjumbe wa Serikali za Mtaa wa Kiburugwa, Kassim Mohamed naye alisema kuwa tangu wampokee Amber Rutty na mpenzi wake, hawajawahi kupokea shtaka lolote la kumvunjia mtu heshima au ugomvi hivyo hata yeye alishangazwa sana na kitendo cha kuona picha hizo.

“Watu wanaweza kumuona kama mtu mkosefu sana lakini kwa kweli hapa mtaani hapana maana sijapokea lalamiko lolote kuhusu yeye labda hivyo tu nilivyovisikia kwenye mtandao basi,” alisema mjumbe huyo.

BABA AMBER RUTTY Afunguka MAZITO

Comments are closed.