The House of Favourite Newspapers

MUSUKUMA Ataka Bangi Iuzwe, ‘Awachamba’ Maprofesa Mdahalo wa JPM- VIDEO

Mbunge Joseph Kasheku ‘Msukuma’ akichangia bungeni Dodoma, leo Novemba 9, ameishauri serikali iruhusu kilimo cha bangi, awataka watalamu na watafiti waeleze madhara yaliyoko kwenye bangi na kutolea mfano baadhi ya nchi zilizoruhusu matumizi ya bangi.

 

Awali, akizungumzia kilimo na uwekezaji ameishanga serikali kwa kuhangaika na mbaazi na kuwaachia wawekezaji jukumu zito la kuuza dhahabu na kuishauri Serikali badala ya kuweka korosho na mbaazi stock wanatakiwa kuweka dhabahu kwani haishuki thamani.

 

Mhe. Msukuma aligusia pia suala la ubora wa viwanja vya ndege akitolea mfano kiwanja cha ndege mwanza. Mbunge huyo amedai kiwanja hicho kinatia aibu upande wa chumba cha wasafiri wa kawaida ambacho ni kidogo na kina sababisha msongamano mara kwa mara.

 

Aidha, Msukuma ameeleza kushangazwa na baadhi ya maprofesa nchini kuchambua hotuba za Rais Magufuli wakati wa Kongamano la Maendeleo ya Uchumi na Siasa lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es salaam hivi karibuni badala ya kueleza namna ambavyo uchumi umekuwa na mambo yapi ya kufanya ili kuuinua zaidi.

VIDEO: MSUKUMA AKIFUNGUKA

Comments are closed.