Amnunulia Mwanaye Airbus A350-1000 Mbili Kimakosa

BILIONEA mmoja nchini Saudi Arabia amenunua ndege mbili aina ya Airbus A350-1000 kwa bahati mbaya wakati akitafuta zawadi ya ‘birthday’ kwa ajili ya mwanaye kupitia njia ya mtandaoni.

 

Bilionea huyo anayefanya kazi katika Wizara ya Nishati nchini Saudi Arabia, amesema kuwa mtoto wake anapenda sana usafiri wa anga, hivyo aliamua kumtafutia zawadi ya ndege za Toy kwa ajili ya kuchezea.

 

Jamaa huyo amesema alipoingia kwenye website ya Airbus alipewa fomu yenye maswali mengi kwa lugha ya Kiingereza, kitu ambacho kilimboa kwa sababu hajui vizuri lugha hiyo, lakini alipochunguza bei aliona imewekwa kwa mfumo wa Dola (USD), na aliona ni fedha ndogo ambayo anaweza kulipia.

 

Bilionea huyo aliamua kufanya malipo ya awali kwa ajili ya kutengenezewa ndege hiyo na baada ya miezi michache, alipigiwa simu na kutumiwa e-mail na watu wa Airbus, akiambiwa kuwa ndege zote mbili zipo tayari kinachohitajika ni rubani wa kuzisafirisha.

 

Mpaka sasa ndege zote mbili amezipokea, moja amemzawadia mtoto wake na moja ameiweka kwa ajili ya matumizi ya familia.

 

Ndege aina ya Airbus A350-1000 inauzwa kwa wastani wa Tsh. bilioni 844.1 kwa ndege moja. Yaani ni sawa na 2.6% ya Bajeti Kuu ya Tanzania 2019/20. Ndege hizi zilianza kuundwa mwaka 2010 na kuingia sokoni mwezi Januari mwaka 2015.   Hadi kufikia Julai 31, 2019 ndege 295 za aina hiyo zilikuwa zimeundwa.


Loading...

Toa comment