BABA AMPA OMBI MAALUM DIAMOND

Abdul Jumaa

Baba wa Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa ametoa ombi kwa mtoto wake baada ya kutangaza rasmi kuwa anatarajia kuoa mwakani kwamba amualike kwenye harusi yake kama njia moja ya kuonesha heshima kwake.  

 

Hivi karibuni msanii Diamond alitangaza rasmi kwenye mitandao ya kijamii dhamira yake ya kumuoa mrembo kutoka nchini Kenya, Tanasha Donna ‘Zahara Zaire’ ifikapo Februari mwakani na kufanya watu wengi kuwa na hamu ya kushuhudia harusi hiyo.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Baba Diamond alisema japo hajapewa taarifa rasmi juu ya dhumuni la mwanaye kutaka kuoa lakini anatamani mwanaye ampe heshima ya kumualika katika siku yake hiyo muhimu.

 

“Sijaambiwa habari za ndoa ila nasikia tu watu mitaani wanazungumzia suala hilo, kikubwa naomba iwe ya heri Mungu afanikishe nitafurahi sana mwanangu akioa lakini namuomba sana asiache kunialika, asiponialika nitaona amenidharau sana, nitajisikia vibaya,’’ alisema Baba Diamond.

STORI: SHAMUMA AWADHI

SHILOLE Afunguka! Mjengo Wake Mpya “Nina Tattoo 17”

Loading...

Toa comment