The House of Favourite Newspapers

Simba, Yanga Zapewa Vibonde FA

ROO ya mechi za FA, zimepangwa Ji­jini Dar es Salaam na kushuhudia timu 64 zikipangwa kwenye makundi mawili ya A na B.

Timu hizo ni za Ligi Kuu,Daraja  la Kwanza,Daraja la Pili na washindi wa FA mikoa.

Yanga itakutana na mshindi kati ya Ihefu na Tukuyu Stars zote za Mbeya ambazo zitache­za Jumamosi hii.

Simba watavaana na timu ya Mashujaa FC kutoka Kigoma huku Ruvu Shooting wakimen­yana na mshindi kati ya Muccoba FC na El­ephant FC kutoka Iringa.

Mechi hizo ambazo zitahusisha vigogo zita­pigwa kuanzia Desemba 21 na 24 huku michezo takribani 32 ikifanyika mwezi huu.

Shughuli ya kupanga makundi iliongozwa na viongozi wa TFF jana ambapo Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten ali­kumbukia walivyowatoa Ihefu kwa penalti msimu uliopita baada ya kwenda nao sare.

Azam FC atacheza na mshindi dhidi ya Madini na Stand Babati.

Comments are closed.