The House of Favourite Newspapers

Baba Askofu Ludovic Minde Ahudhuria Mkutano wa Sinodi ya Maaskofu 2021-2023

0
Baba Askofu Ludovic Minde akizungumza kwenye mkutano huo.

 

 

LEO Machi 2 katika nyumba ya mapadri lenguo Halmashauri ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro, Baba Askofu Ludovic Minde amehudhuria mkutano wa Sinodi ya maaskofu 2021-2023 kwa kuwasikiliza na kupokea maoni kutoka kwa wawakilishi ngazi ya kanisa.

Sehemu ya washiriki.

 

Ngazi hizo ni kuanzia jumuiya ndogondogo, kanisa, wazee wa kanisa, mapadri, masister watoto, wazee vijana na kadhalika Sinodi ya maaskofu 2021-2023 ni kutembea pamoja kupendana kusikilizana kuheshimiana na hivyo kushirikiana kwa pamoja kujenga kanisa.

Baba Askofu akizungumza na washiriki.

 

 

Lengo la sinodi hii ya maaskofu ni kwenda pamoja hivyo askofu husikiliza na kuchukua maoni hayo na kuyapeleka mbele katika mkutano wa maaskofu kitaifa kadhalika kiafrika na hadi kufikia kanisa laki ulimwenguni.

Picha ya pamoja ya washiriki wa sinodi hiyo.

 

 

Moja ya maswali na majibu ni kwa namba gani huduma za kiroho kwa maskini huwafikia bila ubaguzi wanawake na vijana wanasikilizwa kwa namna gani katika jamii.

 

Ni nini mchango wa maadhimisho ya fumbo la ekarist takatifu katika kanisa pia inafundisha jamii isiruhusu ujinga ututawale hasa katika sulala la malezi.

HABARI/PICHA NA ISAAC MAKOI /GPL MOSHI

Leave A Reply