The House of Favourite Newspapers

BABA DIAMOND AMEBAKI JINA TU!

MASKINI! Baba mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma kwa mara ya kwanza amefunguka kwamba yeye kwa mwanaye huyo limebaki jina tu na siyo mzazi tena kama ambavyo watu wengi wamezoea.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, mzee huyo alisema hivi karibuni aliona kwenye mitandao ya kijamii jinsi kijana wake anavyoyafurahia maisha pamoja na ndugu zake wengine ambao ni mama yake mzazi, Sanura Kasim ‘Bi Sandra’, dada yake Diamond, Esma Khan na watu wengine, kitendo ambacho kinaonesha wazi kuwa alikuwa hataki na baba yake mzazi awepo kwani hakumualika.

 

“Unajua mimi na ile familia siyo kitu kimoja kabisa, nimeona kwenye mitandao ya kijamii wakila bata kwenye mjengo mpya aliohamia Diamond huku akiwa na mpenzi wake mpya huyo Tanasha (Donna), lakini mimi sikupewa mwaliko wowote ule, lakini hata hivyo hili jambo halinipi shida kabisa kwa sababu hivi sasa mimi na Diamond limebaki jina tu, yaani mimi najua kama nina mtoto anaitwa Diamond na yeye anajua kuwa ana baba ambaye ndiye mimi, lakini hatushirikishani kwenye mambo yetu,” alisema mzee huyo.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.