The House of Favourite Newspapers

BABA DIMPOZ AMCHAGULIA MKE MWANAYE

Ommy Dimpoz’

BABA mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, Faraji Nyembo ameibuka na kumchagulia mwanaye mke atakapofikia wakati wa kuingia kwenye ndoa.  

 

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa njia ya simu akiwa Sumbawanga alikohamia kwa sasa, baba Dimpoz alisema vijana wengi siku hizi wamekuwa wakiwachagua wanawake wa kuoa kwa kuangalia maumbile ya nje, jambo ambalo siyo sawa kwani watajikuta wanajuta baadaye wakishaingia kwenye ndoa.

 

Aliendelea kusema kwa upande wa mwanaye Dimpoz anamshauri akifikia muda wa kuoa aangalie mwanamke mwenye hofu ya Mungu, yaani mcha Mungu, mwenye akili ya maisha, busara na familia anayotokea na asiangalie shepu na sura kwani atakuja kujilaumu baadaye.

 

“Unajua Dimpoz kwa mama yake yuko peke yake na mama yake alishafariki dunia hivyo anatakiwa akitaka kuoa amtafute mwanamke mwenye hofu ya Mungu ambaye atakuwa faraja kwake, atakuwa mke bora pia kwa upande mwingine awe kama mama kwake na asiangalie shepu, sura au ustaa.

 

“Tatizo la vijana wa siku hizi wanapenda sana kuangalia sura na shepu hata wakishauriwa vipi wanaona ni ujinga, lakini cha muhimu wanachotakiwa kuangalia wanapochagua wake waangalie wacha Mungu na wenye tabia njema,” alisema baba Dimpoz.

 

Kwa upande mwingine baba Dimpoz alimtaka pamoja na sifa hizo alizompa anatakiwa kumuomba Mungu mno kwani kwa macho na akili hawezi kufanikisha jambo lolote bali atajikuta akijilaumu kila siku kwenye ndoa.

Stori:GLADNESS MALLYA, RISASI MCHANGANYIKO

LAVALAVA: “Diamond Ana Mapungufu / Tunavumilia / Alikiba…”

Comments are closed.