The House of Favourite Newspapers

Baba Levo: Udiwani Hauna Mtonyo Labda Uibe

0

DIWANI wa Kata ya Mwanga – Kaskazini katika Jimbo la Kigoma-Mjini kwa leseni ya ACT-Wazalendo ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na vichekesho, Clayton Revocatus ‘Baba Levo’, amefunguka kuwa, nafasi hiyo anayoitumikia ya udiwani haina mtonyo wa kujitajirisha na kama kuna diwani tajiri, basi atakuwa anawaibia wananchi.

 

Baba Levo aliiambia Showbiz Xtra kuwa, udiwani ni wadhifa tu hivyo ukimuona diwani aliyetajirika kwa kazi hiyo, atakuwa ni mwizi.

 

“Ni kazi ya kuwatumikia wananchi, haina mtonyo mrefu kama wengine wanavyodhani, ukiona mtu ametajirikia humo, ujue huyo ni mwizi, anawaibia wananchi wake,” alisema Baba Levo.

Mzee Majuto Awajibu Waliomzushia Kifo, Tazama Video Hii

Leave A Reply