Baba Mkwe Amchomoa Tshishimbi Yanga, Amrudisha CONGO

Kiungo mkabaji wa Yanga Mkongomani, Papy Tshishimbi.

 

AKIWA kwenye msafara wa timu uliokwenda Arusha, kiungo mkabaji wa Yanga Mkongomani, Papy Tshishimbi ameondolewa dakika za mwisho baada ya kupata msiba wa baba mkwe.

 

Kiungo huyo alikuwa sehemu ya msafara wa wachezaji 18 uliosafiri kwenda Arusha kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa leo Alhamisi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

 

Yanga wanatarajiwa kujitupa uwanjani bila ya kiungo na wachezaji wengine wanne Raphael Daudi, Thabani Kamusoko, Andrew Vicent ‘Dante’ wenye majeraha ya goti na Feisal Salim ‘Fei Toto’.

 

Akizungumza na Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh alisema kiungo huyo akiwa katika maandalizi ya safari ya Arusha alipokea taarifa ya kifo cha mkwe na kuomba ruhusa ya kusafiri kwa mazishi.

STORI NA WILBERT MOLANDI | SPOTI XTRA

Loading...

Toa comment