The House of Favourite Newspapers

Baba Mkwe wa Kikwete Azikwa Makaburi ya Kisutu – Video + Pichaz

MWILI wa Baba Mkwe wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rashid Mkwachu aliyefariki dunia jana Alhamisi umezikwa leo katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

 

Viongozi mbalimbali waandamizi na wastaafu wamejitokeza katika kumsindikiza Mzee Mkwachu ambaye ni Baba Mzazi wa Mke wa Kikwete, Mama Salma Kikwete katika safari yake ya mwisho hapa duniani.

Baadhi ya viongozi hao ni Mkwe wa Marehemu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, mjukuu wa Marehemu ambaye pia ni Mbunge wa chalinze, Ridhiwani Kikwete, Rais Mstaafu, Mzee Ali Hassani Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Mizengo Pinda, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar mstaafu, Said Meck Sadick, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar mstaafu, Suleimani Kova, Wabunge, Freeman Mbowe, Zitto Kabwe, Mufti wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi Bin Ally, Shehe Mkuu wa Dar, Sheikh Alhadi Mussa na wengine.

Picha na Richard Bukos | Gpl

FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.