Baba: Msuva hawezi kusaini Simba SC

Mshambuliaji wa Difaa El Jadida, Simon Msuva.

BABA mzazi wa kiungo mshambuliaji wa Difaa El Jadida, Simon Msuva, Mzee Happygod Msuva amesema mwanae hawezi kuja Simba ni uzushi tu wa kujifurahisha kwenye WhatsApp.

 

“Unajua Msuva kule El Jadida ndio mchezaji tegemeo kubwa kama ilivyokuwa Yanga, hivyo si rahisi kurudi huku Tanzania kuja kuichezea Simba haiwezekani, hizo ni taarifa za uzushi tu ambazo watu wanazieleza juu yake.

 

“Nimezungumza nae amenieleza kuwa hakuna kitu kama hicho kwa upande wake na wala hajawahi kuzungumza na Simba hata siku moja.

 

 

“Kwa sasa yeye mipango yake ni kuona anafanikiwa kusonga mbele zaidi katika nchi za Ulaya kwa kuwa kuna mipango ambayo inafanyika kuna timu kutoka nchi mbili tofauti zimejitokeza na anafanya nazo mazungumzo mipango ikikamilika atakwenda huko,” alisema Mzee Msuva.

 

Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na Simba huku leo ikiwa ndio mwisho wa usajili wa faini wa Ligi ya Mabingwa Afrika na Simba wamesisitiza watashtua.


Loading...

Toa comment