The House of Favourite Newspapers

Baba P… Baba Pili… Baba Pilima!-10

0

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA:
“Eti anakuuliza wewe nani?” aliuliza yule abiria akiwa ameinama kidogo ili amuone vizuri yule abiria…

“Anasema anaitwa baba Pili,” yule abiria alimwambia mama Pilima.
Mama Pilima akatembea kwa kasi hadi mlangoni mwa gari…
“Mzima baba Pili?”
“Mzima, twende nikupe lifti.”
SHUKA NAYO MWENYEWE SASA…

Mama Pilima alijikuta akizama ndani ya gari hilo huku akisema…
“Kwani we unakwenda wapi?”
“Mbelembele kule…wewe unakwenda wapi?” alisema baba Pili…
“Nakwenda mahali mara moja.”

“Kufanya nini mama Pilima?”
“Kumwona mama mmoja hivi ni rafiki yangu, nimemmisi sana, nikasema leo niende…”
“Mh!”
“Mbona umeguna baba Pili?”
“Kumwona mama mmoja hivi…”
“Kwani uongo?”

“Wewe ndiyo unayejua…nakusikiliza zaidi wewe.”
“Ndiyo hivyo, labda kama huamini.”
“Nusu naamini.”
“Kwa nini?”

“Kwa vile umesema wewe… lakini mama Pilima ni kwa nini hutaki kuonana na mimi ghafla tu?” aliuliza baba Pilima huku akimkazia macho mwanamke huyo…
“Siyo sitaki bwana…mambo yanaingiliana kidogo,” alijitetea mama Pilima huku macho yakiangalia nje…

“Ndiyo unikache mpenzi wangu? Ilifika mahali nilijiuliza labda kuna kosa mahali.”
“Hamna kosa.”
“Kama kweli hamna kosa, basi tukakae mahali tuzungumze. Huyo mama najua unaweza kumwambia umebanwa, utaonana naye hata kesho.”

Mama Pilima aliguna, akaachia tabasamu huku moyoni akisema…
“Da! Nimebanwa. Ningejua ningetoa sababu nyingine kabisa kuliko kumwambia kuna mtu nimemmisi.”

“Wapi?” aliuliza mama Pilima…
“Popote pale. Lakini penye utulivu wa hali ya juu.”
“Oke, twende.”
Baba Pili aliendesha gari mpaka kwenye baa moja iliyopo kwenye hoteli maarufu, wakashuka hapo…
“Hapa naamini pana utulivu wa hali ya juu,” alisema baba Pili akiwa amemshika mkono mwanamke huyo.

Ilikuwa baa yenye utulivu wa hali ya juu. Wateja wengi walionekana si wale wa fujofujo. Wale waliokuwa na wenza wao, walikuwa wameinamiana wakizungumza kwa karibu ili mazungumzo yao yasisikike kwa wengine.

Baba Pili na mama Pilima walikwenda kukaa kwenye kona moja karibu na ukuta ambapo isingekuwa rahisi mtu aliyekuwa akiingia kuwaona…
“Hapa panafaa,” alisema mama Pilima huku akivuta kiti na kukaa. Wakati wakiingia, baadhi ya wateja, wake kwa waume walimtupia macho mama Pilima kwa jinsi umbo lake lilivyokuwa na mvuto. Wenyewe wanaita figa namba 8!

Wengine waliokuwa wakimtumbulia macho ni wanawake wenzake. Hali hiyo ilimfanya baba Pili azidi kuumia akiamini alifanya makosa makubwa sana kumwacha mwanamke huyo kwa zile siku za mwanzomwanzo…

“Nikimkosa leo, nitajilaumu sana. yaani huu mzigo wote niushindwe mimi kweli? Haiwezekani,” alisema moyoni baba Pili. Hapo sasa wameshakaa.
Walianza kunywa huku wakizungumza kwa kufuata mazingira waliyoyakuta. Maongezi yao ni kwa chini sana…

“Lakini mama Pilima, wewe ulijua wazi kwamba nakupenda sana. kwa nini sasa unitende vile? Yaani ni kama ulinionjesha mahaba yako kisha ukaingia mitini. Umekuwa ukinisababishia kukosa usingizi kiasi kwamba, najuta kukufahamu. Hata pale baa ilibidi niache kwenda, maana ningekuwa nakukumbuka wewe,” alisema baba Pili huku macho yake ya kiume yakikumbana na macho ya kulegea ya mama Pilima hali iliyozidi kumpa hamasa ya mahaba mwanaume huyo…

“Eee! Unajua kusema ule ukweli ni kama nilivyokwambia awali…kuna mambo yaliingilia kati mpaka nikawa siwezi tena kukaa baa jioni, nikitoka kwenye shughuli zangu ni nyumbani tu…”

“Sasa hayo mambo yameisha?” aliuliza baba Pili…
“Kwa mbali saana.”
Mara, mama Pili aliomba kwenda chooni, akavuta simu yake na kuiweka jirani na simu ya baba Pili, akaenda.

Huku nyuma, baba Pilima feki akapiga simu ili kujua mwanamke huyo amefikia wapi! Baba Pili alipoitumbulia macho, moyo ukamlipuka…lip!
“Da! Noma, mzee anapiga,” alisema mwenyewe huku akiangalia mlango wa chooni. Aliishika simu na kuigeuzageuza mpaka mama Pilima alipotoka. Baba Pili aliinua mkono juu kuashiria kwamba, simu yake inaita.

Mama Pilima alitembea kwa kasi mpaka pale…
“Ni nani?” aliuliza.
“Mista,” alisema baba Pili.
Mama Pilima alipoangalia jina, akajua ni baba Pilima feki kwani mumewe amemsevu kwa jina la My Husband!!

“Mbona hupokei?” aliuliza baba Pili…

“Ah! Achana naye huyu, tuendelee na yetu,” alijibu mama Pilima…
“Yetu ninayotaka kuendelea na wewe ni kukuomba twende tukachukue chumba hotelini japo kwa leo tu, naami nitafurahi sana kama utanikubalia.”
Je, unajua nini kilitokea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Ijumaa, siku ya Ijumaa.

Leave A Reply